Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujerumani hasira zao kwa VAR

Japan Vs Spain Ujerumani hasira zao kwa VAR

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ujerumani imechukizwa na bao la utata la Japan dhidi ya Hispania, ambalo lilisababisha kutolewa kwao katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia.

Japan ilifanikiwa kutinga katika hatua ya mtoano ya timu 16 kwa mabao mawili iliyoyapata katika kipindi cha pili dhidi ya Hispania na kuishangaza miamba hiyo ya Ulaya.

La Roja ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Alvaro Morata na kuonekana ikitinga hatua ya mtoano kirahisi pamoja nja Ujerumani, ambayo ilikuwa inaongoza dhidi ya Costa Rica katika Kundi E.

Hata hivyo, Japan ilijipanga na kurudi kipindi cha pili kwa nguvu na kupata mabao mawili kupitia kwa Ritsu Doan na Ao Tanaka na kufanya mchezo kuwa mgumu.

Korosi ambayo ilisababisha bao la pili ilionekana kama mpira ulishatoka nje ya uwanja, kulikuwa na kila dalili kwamba bao hilo lingekataliwa.

Waamuzi ambao walikuwa upande wa VAR walilikubali bao hilo, wakati waamuzi waliokuwa uwanjani wakilikataa kwa kudai kuwa mpira ulishatoka, uamuzi wa VAR ukasimama na kuipa Japan uongozi.

Teknolojia ilithibitisha kwamba mpira ulikuwa uwanjani kutokana na milimita chache kuonyesha bao ulikuwa umegusa mstari kabla ya Kaoru Mitoma kuurudisha uwanjani.

Picha za mnato zilionyesha kuwa mpira huo ulikuwa umetoka nje ya nmstari, huku kukiwa na wachezaji wachache waliokuwa wakilalamikia uamuzi wa mwamuzi wa kati aliyekataa bao awali.

Kabla ya uamuzi wa VAR, mtangazaji wa ITV, Ally McCoist alisema: “Nadhani mpira ulishatoka nje ya uwanja, hivi ndivyo ninavyoamini mimi.”

Chanzo: Mwanaspoti