Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujerumani, England zang'ara UEFA

Top 16 Ujerumani, England zang'ara UEFA

Thu, 3 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi ya Ujerumani na Ligi ya England zimeng’ara hapo jana kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kila ligi kupeleka timu nne katika hatua ya 16 bora kuliko ligi yoyote barani Ulaya.

Ujerumani imetoa timu nne ambapo timu hizo ni Bayern Munich, Borrusia Dortmund, RB Leipzig na Eintracht Frankfurt.

Ambapo kwa upande wa Frankfurt ambae alikuwa kundi D ilibidi acheze mechi zote 6 ndipo ajihakikishie kufuzu hatua inayofuata baada ya kumtandika Sporting ya Ureno.

Uingereza timu nne ambazo zimefuzu hatua ya 16 bora ni pamoja na Liverpool, Chelsea, Manchester City na Tottenham Spurs ambaye nae pia alikuwa kundi D ambalo alitakiwa akamilishe mechi zote 6 aweze kufuzu huku kundi hili likionekana kuwa kila mmoja alikuwa na nafasi ya kufuzu.

Timu ambazo sasa kwa ujumla zimeenda hatua ya 16 bora ni pamoja na Bayern Munich, RB Leipzig, Eintracht Frankfurt, Borrusia Dortmund, Chelsea, Manchester City, Liverpool, Tottenham Spurs, PSG, Benfica, FC Porto, Club Brugge, Intermilan, Napoli, AC Milan pamoja na Real Madrid.

Hivyo basi timu za Ujerumani zipo nne, Uingereza nne, Uhispania moja, Italia tatu, Ufaransa 1, Ureno mbili, Ubelgiji moja.

Timu ambazo sasa zimeshindwa kufuzu hatu ya 16 bora na zinaenda kushiriki michuano ya Europa ni pamoja na Bayer Leverkusen, Barcelona, Ajax, Sporting CP, FC Salzburg, Shakhtar Donetsk, Sevilla na Juventus.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live