Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uingereza yamfungashia virago kocha Southgate

Gareth Southgatee Uingereza yamfungashia virago kocha Southgate

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka nchini Uingereza FA limethibitisha kuachana na kocha wao Gareth Southgate ikiwa ni siku moja tu baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la UEFA Euro 2024 kwa kukubali kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Hispania kwenye mchezo wa fainali mjini Berlin nchini Ujerumani.

Southgate mwenye umri wa miaka 53 amehudumu kama kocha wa timu ya Uingereza kwa miaka nane (8) akiliongoza benchi kwenye mechi 102 na kuifikisha kwenye fainali mbili za EURO pamoja na nusu fainali ya kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Mtendaji mkuu wa FA, Mark Bullingham anasema England inalenga kuwa na meneja mpya "haraka iwezekanavyo" lakini bosi wa muda atakuwa tayari "ikihitajika" kwa kampeni ya UEFA Nations League, ambayo itaanza dhidi ya Jamhuri ya Ireland Jumamosi Septemba 7.

Bullingham alisema: "Mchakato wa kumteua mrithi wa Gareth sasa unaendelea na tunalenga meneja wetu mpya athibitishwe haraka iwezekanavyo. Tunajua kutakuwa na uvumi usioepukika, lakini hatutatoa maoni zaidi juu ya mchakato wetu hadi tutakapomteua."

Southgate mwenyewe amesema; “Najivunia kuwa Muingereza,ni heshima kubwa kwenye maisha yangu kuichezea England na kuifundisha England lakini kwa sasa ni muda wa mabadiliko na ukurasa mpya ndani ya timu.”

Mechi zijazo za England (all Nations League)

September 7: vs Republic of Ireland (a)

September 10: vs Finland (h)

October 10: vs Greece (h)

October 13: vs Finland (a)

November 14: vs Greece (a)

November 17: vs Republic of Ireland (h)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live