Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhuru Selemani kwenye Ramadhan Cup

Uhuru Selemani Mwambungu Uhuru Selemani Mwambungu.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uhuru Selemani Mwambungu jana ameonekana akizima kwenye mashindano ya Silent Ocean Ramadhan Cup akiwa na timu yake ya JEFAG ICD FC.

Katika mchezo huo wa Kundi A ambao ulizikutanisha Jefag ICD FC dhidi ya Al Mahara FC, Uhuru Selemani timu yake [Jefag ICD FC] ilipoteza mchezo baada ya kufungwa goli 1-0.

Uhuru Selemani ni mchezaji mwenye wasifu ‘profile’ kubwa kwenye mpira wa Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.

Amecheza Ligi Kuu ya Tanzania akiwa na Coastal Union, Mtibwa Sugar, Simba, Mwadui FC, Bishara United, amewahi pia kucheza timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars.’

Nje ya Tanzania amewahi kucjeza Saint-Eloi Lupopo [DR Congo] Royal Eagles [Afrika Kusini], Mthatha Bucks [Afrika Kusini], Uniao Desportiva Songo [Msumbiji].

Kwa hiyo Uhuru Selemani kushiriki kwenye mashindano ya Silent Ocean Ramadhan Cup kunaweza kuhamasisha vijana anaokutananao kwenye mechi za mashindano hayo kutamani kufika kwenye level aliyofika.

Vijana ambao kwa sasa wanajitafuta wanaweza kujifunza vitu vingi kutoka kwake lakini pia kuomba ushauri kwa Uhuru Selemani ili kujua ni njia gani za kupita kufikia ndoto zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live