Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhuru Selemani: Lomalisa beki wa kawaida sana

Lomalisa Bnm Joyce Lomalisa Mutambala.

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani Klabu ya Simba, Uhuru Seleman Mwambungu amesema kuwa beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa ni beki wa kawaida sana tofauti na watu wnavyomdhania.

"Nashangaa sana mawinga wa sasa hivi wana kila kitu cha kujiandaa katika mazoezi ili atimie kuwa hatari uwanjani, lakini akikutana na fullback kama Lomalisa anarudi nyuma.

"Sisi wakati damu inaruhusu tunakabwa na mafullback mbavu afu yako fit kinoma kama kina Mbuyu Twite, lakini bado mwendo ulikuwa mdundo wakikaa watatu unawafanya kama group la WhatsApp wewe ndio admin.

"Wadogo zetu hebu badilikeni acheni usela mpira ni kazi sasa nyie hampumziki, hamlali kwa wakati. Mimi hata hivi nilivyo beki kama Lomalisa hawezi kunizuia akienda kupiga krosi atanikuta narudi kupiga krosi Amri Kiemba," amesema Uhuru Seleman.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live