Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhondo wa Derby upo Championship

FRDTRTR Uhondo wa Derby upo Championship

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya jana kushuhudia michezo miwili ikipigwa kati ya Polisi Tanzania iliyokuwa inaikaribisha FGA Talents huku Cosmopolitan ikicheza na Pan Africans, ligi hiyo inaendelea tena leo kwa timu sita kuwasha moto katika viwanja vitatu.

TMA iliyoichapa Pan Africans mabao 2-1 itakuwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kupambana na ndugu zao Mbuni ambayo mchezo wa mwisho ilishinda pia 2-1 ikiwa ugenini Dar es Salaam dhidi ya Cosmopolitan.

Pamba Jiji baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Biashara United itakuwa kwenye Uwanja wake wa Nyamagana jijini Mwanza kucheza na majirani zao Copco FC ambayo ilichapwa mabao 2-1 na ‘Chama la Wana’ Stand United.

Mchezo wa mwisho leo utapigwa Mbeya ambapo Mbeya City iliyoifunga Ruvu Shooting bao 1-0, itacheza na KenGold kwenye Uwanja wa Sokoine huku ikiwa pia na kumbukumbu ya kuchezea kichapo cha 1-0 kutoka kwa Mbeya Kwanza.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo mitatu kupigwa ambapo Biashara United iliyotoka sare ya 1-1 na Pamba Jiji itaikaribisha Stand United iliyoichapa Copco FC mabao 2-1, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Mara.

Vita itahamia kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ambako Green Warriors itawakaribisha Maafande wenzao wa Transit Camp huku mchezo wa mwisho ni kati ya Mbeya Kwanza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Mtwara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Mkuu wa Transit Camp, Said Lyakuka alisema kadri ambavyo ligi hiyo inazidi kusonga mbele ndio ushindani unaongezeka hivyo jambo muhimu ni kukusanya tu pointi nyingi mapema.

Chanzo: Mwanaspoti