Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uholanzi watinga Robo Fainali Kombe la Dunia

Holland Wachezaji wa Uholanzi wakishangilia kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Uholanzi imekuwa timu ya kwanza kujikatia tiketi ya kucheza Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar.

Uholanzi imetinga hatua hiyo baada ya kuichapa Marekani mabao 3-1 mchezo wa mapema uliopigwa katika Uwanja wa Khalifa International.

Mabao ya Uholanzi yamefungwa na M. Depay 10', D. Blind 45+1' na bao la tatu likipachikwa na D. Dumfries 81.

Bao Pekee la USA limewekwa kambani na H. Wright, na kuhitimisha safari yao kwa mwaka huu.

Mchezo wa pili utakaopigwa leo utawakutanisha Argentina dhidi ya Australia majira ya saa 4:00 Usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live