Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uholanzi mwenyeji Uefa Nations League 2023

Netherlands V Gibraltar   2022 Fifa World Cup Qualifier.jpeg Uholanzi mwenyeji Uefa Nations League 2023

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uholanzi kama taifa limepewa nafasi ya kua mwenyeji wa michuano ya Uefa Nations League kwa mwaka 2023 lwakiwashinda mataifa kadhaa ambayo yalikua yanagombea kua mwenyeji wa michuano hiyo.

Timu ya taifa ya Uholanzi itakua mwenyeji wa michuano hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2019 kwa mara ya kwanza na bingwa alikua timu ya taifa ya Ureno.

Timu hiyo maarufu kama The Oranje wamefanikiwa kuwapiku Ubelgiji,Poland, na Wales ambao walionesha nia ya kuandaa michuano hiyo.

Baada ya timu tatu kuongoza kundi na kufuzu hatua ya mtoano ambazo ni Italia, Croatia, pamoja na Hispania sasa ni wazi Uholanzi watazikaribisha timu hizo katika ardhi yake ya nyumbani katika msimu wa 2022/23 wa michuano hiyo.

Michuano hiyo itaanza hatua ya nusu fainali tarehe 14 na 15 Juni wakati mchujo wa fainali ya michuano ya Uefa Nations League na mshindi wa tatu yatafanyika tarehe 18 mwezi wa sita nchini humo.

Droo ya kubanisha timu nne za mwisho ambazo zimefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kufanyika makao makuu ya shirikisho la soka barani ulaya Uefa katika jiji la Nyon nchini Uswisi mwezi Januari mwakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live