Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhispania yaigaragaza Italia, yatinga Fainali

Spain Beat Italy 001 Ferran Torres akishangilia bao lake dhidi ya Italia

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Uhispania imefanikiwa Kutinga Fainali ya michuano ya Uefa Nation League baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mabingwa wa Ulaya (Euro) Timu ya Taifa ya Italia mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo Octoba 7, kwenye dimba la San Siro.

Mabao ya Uhispania yamewekwa kimiani na mshambuliaji wake Ferran Torres dakika ya 17 na 45 kabla ya kwenda mapumziko huku  nahodha wa Italia katika mchezo huo beki Leonardo Bonucci akioneshwa kadi nyekundu dakika ya 42 kabla ya Lorenzo Pellegrini kufunga bao dakika 83 la kufutia machozi kwa Italia.

Kipigo hicho kimewafanya Uhispania kuvunja rekodi ya Italia ya kucheza michezo 37 mfululizo ya michuano yote bila kufungwa tangu mwaka 2018, rekodi ambayo bado imeshikilia kuwa rekodi ya muda mrefu kwa timu za taifa za wanaume Duniani.

Italia imefungwa kwa mara ya kwanza kwenye mchezo rasmi kwenye uwanja wake wa nyumbani tokea mwaka 1999 wakati ambao wachezaji makinda wa Uhispania sita waliokuwa kwenye mchezo wa jana waliokuwa hawajazaliwa ambao ni Pedro Porro, Ferran Torres, Eric Garcia, Bryan Gil, Yeremia Pino na Gavira ‘Gavi’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live