Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugumu wa ratiba waitikisa Arsenal

Arsenal Msgdh.jpeg Ugumu wa ratiba waitikisa Arsenal

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal inakabiliwa na ratiba ngumu kwelikweli katika harakati za kusaka mataji ya Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Michuano ya Ulaya kwenye hatua ya robo fainali, Arsenal imepangwa kukutana na Bayern Munich.

Kama itashinda dhidi ya miamba hiyo ya Ujerumani, itakuwa na shughuli ya kuwakabili mabingwa watetezi Manchester City au mabingwa wa kihistoria Real Madrid kwenye hatua ya nusu fainali.

Kama Arsenal itapenya kwenye michuano hiyo ya Ulaya, ratiba yao itakuwa ngumu zaidi Aprili.

Kikosi hicho cha Mikel Arteta mechi yao ijayo itakuwa Machi 31, itakapokipiga na Man City uwanjani Etihad kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, bato la mbio za ubingwa.

Ikiingia Aprili, watakuwa na mechi dhidi ya Luton, Brighton na Bayern ile ya mkondo wa kwanza, mechi zote hizo ndani ya wiki moja. Kisha itacheza mechi nyingine tatu ndani ya siku saba, itakapozikabili Aston Villa, Bayern ugenini huko Allianz Arena na Wolves.

Arsenal inakabiliwa na mechi nyingine muhimu ya kuamua ubingwa itakapokipiga na mahasimu wao wa London Kaskazini, Tottenham.

Hapohapo, Arsenal bado ina mechi na Chelsea, ambayo haijatafutiwa tarehe ya kuchezwa, hivyo inaweza kuwa ndani ya hiyo hiyo Aprili baada ya awali kuahirishwa. Inaweza kupangwa kabla ya mechi ya Spurs.

Lakini, mabosi wa Ligi Kuu England wanaweza kuichomeka katikati ya wiki ya kuelekea Mei 13.

Baada ya North London Derby, watakuwa na mechi dhidi ya Bournemouth ambayo inaweza kuchezwa katikati ya mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya endapo kama watafika huko.

Arsenal pia ina mechi ya Old Trafford kwenda kuwakabili Manchester United kabla ya mechi yao ya mwisho kumenyana na Everton.

Wakifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi mchezo huo utapigwa Juni Mosi uwanjani Wembley na huenda ikabiliana na ama Atletico Madrid, Borussia Dortmund, Barcelona au Paris Saint-Germain.

Mashabiki wa Arsenal wameanza kuwa na wasiwasi kutokana na ratiba yao kuzongwa na mechi kubwa tupu.

Shabiki wa moja alisema: “Tumekaangwa.”

Mwingine aliongeza: “Hatuwezi kuvuka kwenye hili tukiwa salama.”

Shabiki wa tatu alishangaza, aliposema: “Hiki ndicho kitu tunachokitaka, Arsenal iwe mshindani tena kwenye timu kubwa, mechi kubwa baada ya mechi kubwa. Nasubiri kwa hamu.”

Chanzo: Mwanaspoti