Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugumu wa dili la Bruno, PSG uko hapa

Bruno Guimaraes Newcastle 860x484 Bruno GuimarĂ£es Rodriguez

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Rasmi kipengele kilichokuwa kinaitaka timu inayohitaji kuvunja mkataba wa kiungo wa Newcastle, Bruno Guimaraes kutoa Pauni 100 milioni dirisha hili kimeshapita muda wake na sasa timu yoyote itakayohitaji saini yake itatakiwa kujadiliana na Newcastle juu ya ofa.

PSG ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kumsajli staa huyu wa kimataifa wa Brazil ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2028.

Hata hivyo, kwa sasa mambo yanaweza kuwa magumu kwao kumsajili sababu timu yake inaweza kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa.

Bruno anatajwa kuwa na mpango wa kutaka kuondoka kujiunga na timu itakayomwezesha kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.

Kwa msimu uliopita staa huyu amecheza mechi 51 za michuano yote, amefunga mabao saba na kutoa asisti 10.

Miamba mbalimbali pia inataka kumsajili hasa inayoshiriki ligi ya Mabingwa Ulaya mahali anakotaka akacheze.

Chanzo: Mwanaspoti