Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda waipania Morocco

Ae5fffa1a51ca65a69e654cc027550b3 Uganda waipania Morocco

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya taifa ya Uganda, The Cranes, lazima iwafunge mabingwa watetezi wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Nyumbani (Chan 2020), Norocco katika mchezo wa Kundi C kama wanataka kufuzu kucheza robo fainali.

Kufuatia sare na kufungwa na Rwanda na Togo, Uganda ina nafasi ya kushinda dhidi ya mabingwa watetezi hao, anasema kocha wa Uganda, The Cranes, Johnathan McKinstry.

Kocha huyo kutoka Kaskazini ya Ireland aliiongoza Rwanda kufika hatua hiyo wakati mashindano hayo yalipofanyika kwenye ardhi ya Rwanda mwaka 2016 akitumaini kuizidi Morocco iliyobanwa na Rwanda.

Hatahivyo, Uganda nayo ilitoka sare na Rwanda katika mchezo wa awali.

“Lengo letu tangu mwanzo lilikuwa kufika mbali katika mashindano haya, “alisema McKinstry baada ya timu hiyo kufungwa 2-1 na Togo.

“Na lengo letu kwa sasa bado ni kufika mbali katika mashindano haya.

McKinstry alikiri kuwa amekatishwa tamaa na mchezo wa Togo, lakini anasema kila mmoja sasa anatakiwa kuangalia mchezo ujao ambao ni muhimu sana dhidi ya Simba wa Milima ya Atlas.

“Watu wamesikitishwa na kila mmoja sasa anazungumza kushindwa, lakini sasa tunataka kuweka vichwa vyetu juu na kujua tunaweza kucheza kiwango cha juu na kusababisha matatizo kwa Morocco.”

Mwaka 2014, Uganda iliifunga Burkina Faso na kutoka sare na Zimbabwe lakini walifungwa 3-1 na Morocco katika michuano ya Chan hatua ya makundi.

Chanzo: habarileo.co.tz