Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda bingwa CECAFA Wanawake

E92c5265d0debc1e4d034551730d32b9 Uganda waibuka Mabingwa CECAFA Wanawake

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Timu ya soka ya wanawake ya Uganda imetwaa ubingwa wa michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) baada ya kuifunga Burundi kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Njeru, Uganda, jana.

Katika mchezo huo wa fainali mabao mawili ya Uganda yalifungwa na Sandra Nabweteme na lingine likafungwa na Fazila Ikwaput wakati bao pekee la Burundi liliwekwa kimiani na Joelle Bukuru.

Ethiopia wamekuwa washindi wa tatu baada ya kuifunga Kilimanjaro Queens kwa mabao 2-1, ambapo mabao hayo yalifungwa na Tadesse Bizuayehu na Turist Lema wakati lile la Kilimanjaro lilifungwa na Oppa Clement na kufikisha mabao saba yaliyomfanya aibuke mfungaji bora wa michuano hiyo.

Licha ya kushika nafasi ya nne, Kilimanjaro Queens imepewa tuzo ya timu yenye nidhamu ambayo ilipokelewa na Oppa na Uganda ikatoa kipa bora Daisy Nakaziro na mchezaji bora Fazila Ikwaput.

Timu nyingine zilizoshiriki katika michuano hiyo iliyoanza Juni Mosi mwaka huu ni Sudan Kusini, Zanzibar, Djibouti na Rwanda ambazo zilitolewa hatua ya makund

Chanzo: www.habarileo.co.tz