Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uganda: Wachezaji, Makocha kufundishwa wimbo wa Taifa

Uganda Cranes XI 2 Timu ya Taifa ya Uganda

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Kandanda nchini Uganda FUFA limesema wachezaji wote watakaokuwa wanaitwa kuunda timu za taifa watalazimika kushiriki ratiba maalum ya kujifunza kuimba wimbo wa taifa hilo.

Kauli ya FUFA inakuja baada ya kuwepo kwa maneno maneno kuwa wachezaji wengi wa Uganda hawaufahamu wimbo wa timu ya taifa, hivyo hawajui kuimba wimbo huo suala linalopelekea wachezaji kukaa kimya wakati wimbo ukiwa unaimbwa.

Mbali na wachezaji, viongozi wote watakaokuwa wanahusika na hizo mechi watatakiwa pia kuwa sehemu ya washiriki wa ratiba ya kujifunza uzalendo kwa kuimba wimbo wa taifa la Uganda.

Takribani makocha 10 wa timu za taifa watafundishwa kuimba, timu za wanawake, timu za kiume na timu za vijana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live