Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaransa yapata pigo lingine

Saliba X Upamecano Ufaransa yapata pigo lingine

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Kylian Mbappe kuvunjika pua na kuripotiwa atafanyiwa upasuaji, Ufaransa imepata pigo lingine baada ya mabeki wao Dayot Upamecano na William Saliba kukosa mazoezi ya Jumatano kutokana na maumivu ya misuli.

Ufaransa ilianza safari yao ya Euro Jumatatu usiku dhidi ya dhidi ya Austria ya kocha wa zamani wa Manchester United, Ralf Rangnick na kuishinda bao 1-0.

Hata hivyo, ushindi huo ulikuwa na maumivu kwani staa wao Mbappe alitoka uwanjani dakika za mwisho huku pua yake ikiwa inavuja damu baada ya kuvunjika.

Ripoti zinaeleza supastaa huyo wa Real Madrid hatocheza mechi ya leo dhidi Uholanzi ingawa anaweza akawepo Jumanne ya wiki ijayo dhidi ya Poland.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa ya kituo cha habari cha Ufaransa L'Equipe Ufaransa inaweza ikawakosa pia mabeki hao wawili.

“Dayot Upamecano na William Saliba, waliocheza pamoja dhidi ya Austria, hajashiriki mazoezi ya Jumatano kwa sababu ya maumivu ya misuli," ilisema ripoti hiyo.

Ikiwa hali za mastaa hawa hazitokuwa sawa hadi kufikia leo asubuhi, kuna uwezekano nafasi zao zikachukuliwa na wachezaji wengine kama Jules Kounde, Ibrahima Konate na Benjamin Pavard ambao wanaweza kucheza maeneo yao kwa ufanisi.

Akiongea Jumanne ya wiki hii kuhusu hali ya majeraha ya Mbappe na wachezaji wengine, Kocha Didier Deschamps alisema; "Jumatano (juzi), atafanyiwa vipimo kuona maendeleo yake na ikiwa ameumia sana wataalamu wa afya watafanya kila liwezekanalo arudi katika hali ya kawaida."

Picha mbalimbali zilimwonyesha Mbappe akiwa mazoezini jana huku kwenye pua yake kukiwa na plasta na inaelezwa hali yake inaendelea vizuri.

Chanzo: Mwanaspoti