Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufaransa watinga Fainali Kombe la Dunia Qatar

France Final Qatar Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia kutinga Fainali ya Kombe la Dunia

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Ufaransa wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Morocco jana Uwanja wa Al Bayt mjini Al Khor nchini Qatar.

Mabao ya Ufaransa yalifungwa na Theo Hernández dakika ya tano tu ya mchezo huo na Randal Kolo Muani dakika ya 79 na kuzima ndoto za Morocco kuweka rekodi mbili kwa mpigo.

Sasa Ufaransa itakutana na Argentina katika Fainali tamu mno Jumapili Uwanja wa Lusail Iconic mjini Lusail.

Nayo Morocco iliyoweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika Nusu Fainali ya Kombe la Dunia itamenyana na Croatia Jumamosi Uwanja wa Khalifa International mjiji Al Rayyan kuwania nafasi ya tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live