Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Ufalme lazima urudi Jangwani" - Manara

Manara FULL MAJIGAMO msemaji wa Yanga, Haji Sunday Manara akiwa katika mkutano na waandishi

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa msimu huu ni wa kurudisha ufalme wao kwenye Ligi Kuu Bara lakini pia kubeba makombe yote yaliyo mbele yao.

Hayo yaesemwa na msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara alisema ushindi katika mechi ya kwanza ya ligi umeonyesha dalili ya klabu hiyo kutwaa ubingwa msimu huu.

"Kwa miaka minne Sasa hatujatwaa ubingwa na katika miaka minne hiyo hiyo mechi zetu zote za kwanza za ligi hatukushinda. Tulitoka sare mechi tatu na kupoteza Moja.

"Mara ya mwisho tumetwaa ubingwa ni msimu wa 2016/2017 na msimu huu tulishinda mechi yetu ya kwanza ya ufunguzi kama tulivyofanya msimu huu hivyo hiyo ni dalili nzuri kuwa msimu huu ubingwa Wetu,"amesema Manara.

Manara amesema haiwezekani wakae misimu  mitano bila ubingwa kwani  wana kikosi Bora sana.

"Msimu ya miaka miaka ya nyuma tumeshawahi kufanya hivyo kuchukua ubingwa mara Tano mfululizo na watani zetu wa jadi walifanya hivyo pia lakini zama hizo hatuwezi kukubali kukaa miaka yote hiyo bila ubingwa.

"Huu ni wakati Wetu.Tumedhamiria kuchukua makombe yote,ikiwemo ligi Kuu, kombe la Shirikisho la Azam na hata Mapinduzi ," amesema Manara na kuongeza

"Hatumaanishi tunawadharau wapinzani wetu, hapana,tunawaheshimu lakini kutokana na mipango ya kikosi chetu, uongozi,wadhamini tunakwenda kushinda ubingwa msimu huu ," amesema Manara.

Hata hivyo Manara amewaambia mashabiki wa klabu hiyo kuwa ligi ni Marathon hivyo wajipange kwa matokeo yoyote kwani hakuna timu Duniani iliyowahi kushinda toka mwanzo Hadi mwisho wa ligi.

Naye Afisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema kikosi chao Kiko vizuri kikiwa tayari kwa mchezo  wa kesho wa ligi dhidi ya Geita Gold.

"Kocha amesema niwaambie kuwa timu Iko vizuri na imejipanga kushinda licha ya kwamba mchezo utakuwa mgumu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz