Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufahamu Uwanja wa Pele Rwanda, Al-Merreikh vs Yanga kupigwa hapa

Amahorostadium1 Ufahamu Uwanja wa Pele Rwanda, Al-Merreikh vs Yanga kupigwa hapa

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwanja wa Pele Kigali Rwanda ndio uwanja ambao utatumika katika mchezo baina ya Al Merreikh dhidi ya Yanga, Al-Merreikh pia waliutumia uwanja huo katika michezo yao ya hatua ya awali na kufuzu kwenda hatua inayofuata.

Ni uwanja ambao upo karibu na jiji la Kigali,n aka bla ya kuitwa Pele Uwanja huo ulikuwa ukijulikana kama Nyamirambo Satdium.Sababu kubwa ya Uwanja huo kubadilishwa jina inatokana na FIFA.

Baada ya kifo cha gwiji wa Soka Duniani, Edson Arantes Dos Nacmento 'Pele' kufariki basi FIFA waliamua kuja na mpango wa kumuenzi gwiji huyo ambaye alikuwa ni alama kubwa ya kuutangaza mchezo wa soka duniani.

Ikumbukwe pia Rais wa FIFA Gian Infaltino alikuwa sehemu ya uzinduzi wa Uwanja huo ambao unachukuwa mashabiki 22,000 akiwa na mwenyeji wake Rais Paul Kagama.

Uzinduzi wa uwanja huo ulikuja mara baada ya mkutano mkuu wa 23 wa FIFA kufanyika KIGALI Rwanda March 23 2023,hivyo mpango wa kuuboresha uwanja huo ulianza kufanyika tangia mwezi January 2022 mpaka kukamilika.

Na baada ya mkutano mkuu kukamilika Rais wa FIFA na Paul Kagame wakiwa na mastaa mbalimbali waliowakilisha mataifa yao haswa wale waliostaafu waliweza kupiga mechi ya kirafiki,mmoja wa mastaa hao ni mwanadada Amanda Dlamin staa wa zamani wa kike wa timu ya taifa ya Afrika Kusin Banyanabanyana.

Picha yao ilitrend sana ya Kagame na Infaltino.

Kwa sasa Uwanja huo unatumiwa na timu za Rayon Sports na APR katika michezo yao ya Ligi kuu na ile michuano ya kimataifa.

Mchezo mkubwa wa kimataifa kwa ngazi ya klabu kufanyika katika Uwanja huo ni kati ya APR Vs PYRAMIDS na Rayon Spots Vs Al Hilal.

Mabibi na Mabwana KIGALI PELE STADIUM inatarajiwa kubebe mchezo mwingine wa kimataifa mkubwa baina ya vigogo Al Merreikh vs Yanga SC kutoka Tanzania.

Wananchi wao wanasema watu 22,000 ni wachache sana na wao peke yao wapo tayari kuujaza Uwanja huo,wanataka kuweka rekodi ya kuujaza uwanja wa ugenini wakati wao sio wenyeji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live