Uefa inabeba "jukumu la msingi" kwa matukio ya mtafaruku ambayo "nusura yasababishe maafa" kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka jana kati ya Liverpool na Real Madrid, inasema ripoti huru.
Mashabiki walishambuliwa na kupigwa mabomu ya machozi nje ya Uwanja wa Stade de France wa Paris huku mchezo wa kwanza ukicheleweshwa kwa dakika 36.
"Inashangaza hakuna mtu aliyepoteza maisha," ilisema ripoti hiyo, ambayo Uefa iliidhinisha baada ya fainali ya Mei 28.
Mamlaka za Uefa na Ufaransa hapo awali zililaumu mashabiki wasio na tikiti kwa hafla hiyo.
Ripoti inasema hakuna "ushahidi" wa kuunga mkono madai "ya kulaumiwa".
"Jopo limepata kuwa Uefa, kama mmiliki wa hafla, inawajibika kwa mapungufu ambayo karibu yasababishe maafa," ilisema ripoti hiyo.
Ingawa ilisema kulikuwa na "kosa la kuchangia" kutoka kwa vyombo vingine - haswa polisi wa Ufaransa na Shirikisho la Soka la Ufaransa - matokeo yalisema shirikisho la Uefa ‘lilikuwa mstari wa mbele".