Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uefa Kufanya Mabadiliko Makubwa 2024

Uefa Presdaa Rais wa UEFA, Aleksander ?eferin

Sat, 14 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Kandanda barani Ulaya (Uefa) limetangaza utaratibu mpya wa mashindano yake yote matatu, huku likisema kuwa mradi wa kuanzisha Super League sasa umezikwa “kwa angalau miaka 20”.

Baada ya kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika jijini Vienna, Austria mwishoni mwa wiki hii, Rais wa Uefa, Aleksander Ceferin alisema baada ya mashauriano ya muda mrefu hatimaye wamefikia uamuzi wa kupanua mashindano hayo matatu kwa kuongeza timu nne na kuondoa hatua ya makundi na kwamba mfumo huo utaanza msimu wa mwaka 2024/25.

Uamuzi huo wa mkutano mkuu ni mwendelezo wa uamuzi uliofanyika Aprili 19 wa kuanzisha mfumo unaoitwa “Swiss system”.

Mabadiliko makubwa katika mfumo huo ni kupunguza idadi ya mechi kutoka 10 hadi nane katika hatua ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kubadili vigezo vya kutoa nafasi mbili kati ya nne za nyongeza za kucheza ligi hiyo kubwa.

“Hii inaonyesha jinsi Uefa inavyoheshimu kanuni za ushindani wa wazi na kupata nafasi kutokana na kufuzu, huku ikitambua haja ya kulinda mashindano ya ndani katika nchi wanachama,” imeandika tovuti ya Uefa.

Mechi nane za Ligi ya Mabingwa zitachezwa ndani ya Wiki Kumi za Ulaya kwa mujibu wa uamuzi wa Aprili, 2021. Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi ya Europa na Ligi ya Conference zitakuwa na wiki pekee katika kalenda ya Uefa.

Nafasi nne zilizopatikana kutokana na kuongeza timu kutoka 32 hadi 36 katika hatua ya ligi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zimewekewa vigezo.

Nafasi moja, kwa mujibu wa uefa.com, itakwenda kwa timu itakayoshika nafasi ya tatu ya mashindano ya nchi ambayo inashika nafasi ya tano katika orodha ya ubora ya nchi wanachama wa Uefa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live