Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Udhamini wa Pilsner umekuja wakati muafaka - CEO Imani Kajula

Udhamini Wa Pilsner Umekuja Wakati Muafaka   CEO Imani Kajula.jpeg Udhamini wa Pilsner umekuja wakati muafaka - CEO Imani Kajula

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Imani Kajula amesema ujio wa udhamini wa bia ya Pilsner Lager utachochea kiasi kikubwa kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa klabu.

Kajula ameitoa kauli hiyo leo Novemba Mosi, 2023 wakati Simba ikiwatangaza wadhamini hao wapya waliongia mkataba wa Shilingi Bil. 1.5 kwa miaka mitatu.

"Ni ubia wa nguvu kabisa, ubia wa Simba wawili. Hii ni package ambayo imekuja wakati mwafaka. Serengeti ni mbia mkubwa sana wa mpira wa Tanzania, huu ni mwendelezo wa kusaidia mpira."

"Udhamini huu utasaidia uendeshaji wa klabu, gharama za uendeshaji wa vilabu huwa ni kubwa. Upatikanaji wa fedha ni muhimu sana. Tunawashukuru kukubali kuungana nasi kama wadhamini wa Simba."- CEO Imani Kajula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live