Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Udhamini sio rahisi kama watu wanavyofikiri

Visit Rwandas.png Udhamini sio rahisi kama watu wanavyofikiri

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maeneo ambayo mkataba wa Rwanda na African Football League unagusa ni pamoja na wachezaji wa timu zote zinazoshiriki mashindano hayo kuvaa jezi zenye neno la VISIT RWANDA kwenye mikono ya jezi zao.

Matangazo ya VISIT RWANDA yataonekana kupitia digital boards za uwanjani, workshop/events mbalimbali ambazo watafanya AFL lazima VISIT RWANDA ionekane. Online broadcasting [media channels] zote za CAF Visit Rwanda lazima ionekane.

Sasa watanzania wengi baada ya kuona Rwanda itatangazwa kupitia African Football League wameibua maswali mengi kwa nini sisi hatukuiona hiyo fursa?

Jambo hili ni la kimkakati sio la kulala na kuamka unaingia, naamini kuna mzigo mkubwa Rwanda wameweka kwenye mashindano haya kupitia Wizara ya Michezo Rwanda, Bodi ya Maendeleo Rwanda, Rwanda Air n.k.

Kwa mfano shirika la ndege la Rwanda lina fika kwenye mataifa 29 duniani ikiwa ni pamoja na miji mikubwa ya kitalii duniani [London, Paris, Doha, Dubai, Brussels, Johannesburg, Dakar, Lagos, Dar n.k].

Kwa hiyo kwa CAF kuingianao makubaliano kwa upade wa shirika la ndege kuna faida nyingi wanazipata ikiwa ni pamoja na kuzisafirisha timu shiriki za AFL kutoka sehemu moja kwenda nyingine, waamuzi na maofisa wengine wa CAF pia watatumia Rwanda air.

Kwa hiyo ukiangalia shirika la Rwanda air na CAF kuingia kama washirika kupitia serikali ya Rwanda na ku-promote vivutio vya Rwanda kuna maeneo mengi yanaguswa kwa hiyo sio kitu ambacho kimetokea tu kwa bahati.

Mambo ya udhamini hususan kwa Serikali au Wizara sio rahisi kama watu wanavyofikiria, lazima iwe kwenye bajeti ya mwaka husika wa fedha. Huwezi kukurupuka tu kwa kuwa mashindano yanafanyika Tanzania basi Bodi ya Utalii Tanzania inaenda kutoa dola za Marekani 100 milioni kudhamini ili kupata nafasi ya kutangaza utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live