Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchunguzi wa unyanyasaji waanzishwa dhidi ya refa maarufu wa soka wa kike

Uchunguzi Wa Unyanyasaji Waanzishwa Dhidi Ya Refa Maarufu Wa Soka Wa Kike Uchunguzi wa unyanyasaji waanzishwa dhidi ya refa maarufu wa soka wa kike

Tue, 24 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Shirikisho la soka Rwanda linachunguza unyanyasaji na jaribio la kushambuliwa na mashabiki dhidi ya refa maarufu wa kike kwenye mchezo wa soka katika ligi ya wanaume nchini humo.

Salima Mukansanga aliongoza mechi ya sare ya 0 – 0 siku ya Jumamosi, kati ya Kiyovu Sport na Gasogi United, lakini "ripoti za mchezo zinaonyesha kwamba alishambuliwa", msemaji wa Shirikisho la soka aliambia BBC.

Watu waliohudhuria mchezo huo waliambia BBC kwamba kundi la mashabiki wa Kiyovu Sport waliimba mara kwa mara wakimwita Bi Mukansanga "kahaba".

"Baada ya mchezo huo wafanyakazi wa usalama walilazimika kuingilia kati kuzuia baadhi yao kumshambulia kimwili" Jules Karangwa, msemaji wa Shirikisho la soka anasema.

Katika barua ya wazi, rais wa mashabiki wa Kiyovu Sport Hemedi Minani alikashifu "unyanyasaji na shambulizi" dhidi ya Bi Mukansanga na kumwomba msamaha.

Hatua zitachukuliwa na kamati ya nidhamu baada ya uchunguzi, afisa wa Shirikisho la soka alisema.

Chanzo: Bbc