Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchambuzi: Ugiriki vs Hispania

Spain 696x464 Kikosi cha Hispania

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi za kutafuta tiketi ya kwenda nchini Qatar 2022 kwaajili ya michuano ya Kombe la Dunia zinaendelea Hispania wataendeleza jitihada za kutafuta kukaa juu kwenye kundi B watakapo safiri kukabiliana na Ugiriki leo usiku.

Sweden ndiyo vinara katika kundi B wakiwa na alama 15 mbele ya Spain ambao wamekusanya jumla ya alama 13 baada ya michezo 6 wakiwa juu ya Ugiriki kwa tofauti ya lama 4.

Taarifa ya Timu

Pantelis Chatzidiakos wa Ugiriki alipokea kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Sweden wakati nahodha Anastaios Bakasetas pia alipata kadi mbili za manjano kwenye mchezo huo hivyo hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo.

Dinos Mavropanos pia hatocheza kwenye mechi za mwezi huu Novemba Van’t Schip anaweza kumuita Dimitris Goutas ambaye ni beki wa kati amefunga mabao manne kwenye Super Lig msimu huu.

Kostas Tsimikas anaweza kuitwa kucheza beki namba tatu kuchukua nafasi ya Petrois Mantalos ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Wakati kwa upande wa Hispania itamkosa mchezaji wake Torres sababu ya jeraha alilopata wakati wa fainali ya Nations League vilevile itawakosa Ansu Fati, Gerrard Moreno, Yeremi Pino na Mikel Oyarzabal.

Pau Torres na Aymeric Laporte watatawala eneo la ulinzi wakati Garcia yupo nje wakati Simon Garcia wakati Simon Garcia atahakikisha hakuna mpira unaingia langoni mwa Spain.

Eric Garcia amelazimika kukosa mechi hii sababu ya majeraha hivyo Alvaro Morata yupo fit kuongoza safu ya ushambuliaji.

Kikosi cha Ugiriki kinachoweza kuanza: Vlachodimos; Androutsos, Goutas, Tzavellas, Tsimikas, Giannoulis; Bouchalakis, Siopis; Mantalos; Pavlidis, Masouras

Kikosi cha Hispania kinachoweza Kuanza: Simon; Carvajal, P. Torres, Laporte, Alba; Koke, Busquets, Gavi; Sarabia, Morata, Olmo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live