Uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini Kenya FKF hautafanyika mwaka 2024 kama ambavyo ilipangwa lakini sasa utafanyika mwaka mmoja mbele.
Ruhusa ya kutofanya uchaguzi umepewa baraka zote na Shirikisho la Kandanda duniani FIFA ambao wameruhusu kuendelea kufanya kazi kwa mwaka mmoja zaidi ili kuweka mipango sawa.
Itakumbukwa uongozi uliopo madarakani kwa hivi sasa ulisimamishwa na Amina Mohammed Waziri zamani wa Michezo kwa kile alichokieleza kuwa ni utovu wa nidhamu na matumizi mbaya ya fedha.
“Tumeongea na FIFA na CAF kuwaomba uchaguzi usogezwe mbele na tayari wamekubaliana nasi na sasa uchaguzi mkuu utafanyika mwaka 2025 badala ya 2024”, kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa.