Mgombea nafasi ya ujumbe ndani ya klabu ya Yanga Omary Kimossa amesema ataitumia vyema taaluma yake ya mambo ya fedha kuzileta ndani ya klabu.
Kimossa amesema Yanga kwa uwezo alionao anaamini akipata nafasi hiyo atasaidiana na wenzake kuisogeza mbele timu hiyo.
"Mimi ni Mtaalamu wa fedha, nimefanya kazi na kusaidia mashirika mengi kupata fedha zinazohitajika kuendesha biashara na kupanua Biashara,"
"Hamu yangu ya kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ilikuja baada ya kuona imefika hatua timu yangu ya Yanga imekwama kabisa kupata fedha kutoka mabenki kwasababu moja au nyingine, nilipojua Rais mtajariwa ana mawazo haya ya kiuwekezaji kwenye maeneo yetu ya Kaunda na Kigamboni, na kutambua kilichotokea nyuma, nimeamua kuja kusaidiana na wenzangu," anasema Kimossa.
Anasema atatumia uwezo wake na nguvu zake kuhakikisha hilo linafanikiwa kama aliivyofanikisha kwa wengine ili Yanga isogee, wasiishie kuchora michoro ya majengo kisha wakakwama.
Aidha Kimossa amewaomba kura Wanayanga ili wakapambane kwa pamoja kuondoa tatizo hilo.