Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubunifu wa Yanga umeanza kuwalipa - Shaffih Dauda

Shaffih D X Bacca Ubunifu wa Yanga umeanza kuwalipa - Shaffih Dauda

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amewapongeza Idara ya Habari ya Klabu ya Yanga kutokana na ubunifu ambao wamekuwa wakiufanya siku hadi siku na kufanya engagement kwa mashabiki zao.

Dauda amesema kuwa utaratibu wa Yanga kuzipa mechi zao za nyumbani za kimataifa majina ya wachezaji wao, zinaongeza hamasa kwa wachezaji, kuwavuta mashabiki na zaidi ni kutengeneza pesa kupitia wadhamini wanaodhamini mechi hizo.

"Yanga wamekuwa wabunifu sana kwenye suala la kuisogeza timu kwa mashabiki ‘fans engagement’, ubinifu huo umeanza kuwalipa kwa sababu sasa hivi wanaingiza pesa kupitia ubunifu huohuo.

"Mtindo wa kuzipa mechi majina ya wachezaji [Max Day, Aziz Ki Day na Bacca Day] umeanza kuwalipa! Jana wameingiza Tsh. 40 milioni kwa ajili ya Bacca Day.

"Kupata fedha ni jambo moja lakini klabu imeendelea kusogezwa kwa watu [wanachama, mashabiki, wafuasi na wadau].

"Ukifatilia hizi kampeni ambazo zinafanywa na Yanga zimewavutia watu wengi sana hadi wale ambao sio mashabiki kabisa wa mpira hususan wa jinsi ya kike.

"Walianza kwenda uwanjani wamechomekea, wakaenda wamebeba fungua sasa wanakuja na msuli, kanzu na hijabu kama ilivyo utamaduni wa Zanzibar. Inavutia kwa weli, na huo ndio ubunifu.

"Na hii ina akisi uongozi wa vijana aina ya kina Eng. Hersi Said na Arafat Haji kwa sababu ulimwengu wa sasa ni wa vijana na unahitaji kwenda wanavyotaka wao [fashion, teknolojia].

"Yanga inaondoka kwenye kuita mashabiki kwa makelele! Wanafanya promotion inayotokana na madhui kitu ambacho watazamaji na wasikilizaji wanakitaka.

"Yanga wamefanya jambo zuri na la kijanja ambalo ndani yake lina promotion campaign na ndio ulimwengu unavyohitaji kwa sasa," amesema Shaffih Dauda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: