Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubunifu na ubora wa goli la Steve Mounie dhidi ya Stars

SOMO STARS Move ya goli alilofungwa Stars dhidi ya Benin

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ilikuwa mbinu bora sana kutumika kwenye dakika ya 71 ambapo Stars ikiwa imepandisha timu juu kwa mabeki wa kati(Mwamnyeto & Job) wakiwa mstari wa juu wa ukabaji(High line of defense) na Kibwana Shomari akiwa juu zaidi katika umbo la ushambuliaji.

Steve Mounie, mfungaji wa goli akiwa kama mshambuliaji kiongozi alitumia dhaifu hilo la Stars kwa kudrop kati na kutanua pembeni mwa uwanja hivyo kufanya kuwa nyuma ya Kibwana.

Ubunifu huu wa kudrop chini na kutanua uwanja kuliwazuia Mwamnyeto na Job kumfuata kwa kuhofia kutoka eneo lao la ukabaji hivyo kumuacha MOUNIE akiwa pekeake hadi alipopokea mpira.

Mounie alipokea mpira akiwa pembeni mwa uwanja peke yake na kufanya mkimbio bingwa (Diagnal Cut in run) kabisa kwa kutoka pembeni mwa uwanja na kuingia kwenye eneo hatarishi kimashambulizi (Halfspace 14 zone) huku akiwa kwenye mwendo wa juu uliomfanya atengeneze gap kati yake na Kibwana aliyeenda kushambulia.

Kasi ya juu ya mkimbiaji iliwachanganya mabeki kutojipanga kwenye umbo sahihi la ukabaji huku kasi ya juu ya upigaji mpira ule uliwahi sekunde kadhaa na kumfanya MANULA achelewe katika kujipanga na kuufuata mpira ule.

Brilliant, masterclass and clinical finishing yake ilichagizwa na speed of play kwa One touch self setting kabla ya kupasia nyavu kwa mpira aliopiga kiufundi kwenye mwamba wa mbali (Far Post) tena ukiwa kwenye spidi ya juu na umbo la mwezi mchanga unaweza kuuita Semi Curled Curve.

Hapa hakuna wa kumlaumu kwakuwa yalikuwa makosa ya timu kiujumla (COLLECTIVE TEAM MISTAKES) bali anapaswa kusifiwa mfungaji kwa mbinu alizotumia kutengeza nafasi isiyoonekana na hatimae kufunga goli lile pekee lililoamua mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live