Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubora wa Yanga unavyoitesa Simba

Simba Vs Yanga Aziz Ki Debut.jpeg Ubora wa Yanga unavyoitesa Simba

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubora wa Yanga kwa sasa utaitesa sana Klabu ya Simba SC kwa nini? Kufungwa (1-5) wameanza kuaminishana ni hujuma, kwamba wachezaji wamehujumu timu. Viongozi wa Simba hawataki kukiri kuwa wamezidiwa ubora na Yanga.

Hiki kirusi cha kutokutaka kukubali ubora wa Yanga kitaleta maafa ndani ya Simba kwa sababu hawatawekeza nguvu kuijenga timu ya ushindani kwa kusajili vizuri, watawekeza nguvu zao kutafuta mchawi.

Wakija kustuka ni too late wenzao watakuwa mbali. Hata wangesimamisha wachezaji kumi (10) hilo sio suluhisho.

Simba imeruhusu magoli kwenye mechi (10) kati ya (12), ni kwamba ilihitajika timu 1 bora kuwafunga magoli mengi kuwakumbusha kuwa timu yao ina upungufu sehemu fulani, jukumu hilo kalifanya Yanga. Huenda dhahama ingetokea hata kwa Al Ahly lakini hawakutumia nafasi walizopata.

Unamsimamisha Clatous Chama kwani lini aliwahi kuwa na performance nzuri dhidi ya Yanga iliyobora? Unamsimamisha Inonga kwa nini usimsifu Aziz Ki, Musonda au Max kwa kufunga magoli ya viwango?

Unamsimamisha Kapombe kwani mara ngapi alifanya makosa hata kabla ya dabi? Baadhi ya viongozi wa juu wanaficha makosa yao ya kusajili kina Ayubu kisha jumba bovu wanawaangushia wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: