Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubora! Gomes, Milton na mageuzi ya kimkakati Simba

20ed5ce3149e244f74bdb045d885d0a2 Ubora! Gomes, Milton na mageuzi ya kimkakati Simba

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroMore by this Author MASHABIKI wa Simba wanacheeka. Kila mmoja ana raha juu ya mwenendo wa timu yao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo imevuna pointi sita katika mechi mbili za kundi A ilizocheza dhidi ya AS Vita ya DR Congo na Al Ahly ya Misri, matokeo yanayoifanya Simba kutanguliza mguu mmoja kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Ujio wa kocha mkuu Didier Gomes na kocha wa makipa, Milton George unatajwa kuwa miongoni mwa siri za mafanikio ya kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Kwa makipa wa Simba, Aishi Manula na Beno Kakolanya, ukiachana na ubora wa viwango vyao kuimarika, lakini kocha Milton ameonekana kuimarisha zaidi maelewano ya makipa hao.

“Makipa wa Simba wamebadilika sana, hasa Aishi amekuwa na mabadiliko, kuna vitu ambavyo bila shaka kocha anayewafundisha sasa amevibadilisha,” anasema kipa nyota wa zamani wa timu hiyo, Mohammed Mwameja.

Anasema siyo kwa Manula pekee, bali hata Kakolanya na kwenye kikosi cha Simba sasa presha ya makipa haipo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz