Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubingwa Ligi Kuu ya Wanawake ni mtifuano

JKT Queens JKT Queens

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kivumbi cha Ligi Kuu ya Wanawake kinaendelea, vita kubwa kwenye ligi hiyo kwa sasa ni mbio za ubingwa ambapo wababe Simba Queens wanachuana vikali na Maafande wa JKT Queens, huku timu hizo zikipokezana usukani wa ligi hiyo kila timu ikiwa imesalia na mchezo mmoja.

JKT Queens leo wameivurumisha Fountan Gate Princess kwa bao 3-0 na kufikisha alama 43 alama moja mbele ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba Queens, magoli ya JKT Queens kwenye mchezo huo yalifungwa na Stumai Abdallah, Happy Mwaipaja na Swaumu Jongo mchezo huo ulipigwa katika dimba la jamhuri jijini Dodoma.

Michezo ya mwisho ya ligi hiyo itapigwa Mei 17 ambapo JKT Queens watakuwa wageni wa vibonde wa ligi hiyo Mkawa Queens wakati Simba Queens wakipapatuana na Ceasiaa Queens.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live