Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubabe! Messi amchapa Ronaldo 5-4

Messi Ronaldo Saudi Ms Ubabe! Messi amchapa Ronaldo 5-4

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wa kirafiki kati ya PSG dhidi ya kombaini ya mastaa wa Al Hilal na Al Nassr umemalizika mjini Riyadh nchini Saudi Arabia ambapo PSG amefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 5-4.

Mchezo huo uliowakutanisha miamba wawili wa soka duniani, Lionel Messi wa PSG na Ronaldo wa Al Nassr ulisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka ulimwenguni kote.

Katika mchezo huo, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufunga magoli mawili (moja la penati dakika ya 34 na jingine dakika ya 45+6') huku Messi akifunga goli moja tu ambalo aliliweka kimyani mapema kabisa dakika ya 3 tu ya mchezo.

Mchezo umemalizika kwa PSG kuibuka na ushindi wa 5-4 dhidi ya combine ya Al Hilal na Al Nassr.

Wengine waliofunga kwa upande wa Al Hilal na Al Nassr ni Hyun-Son dakika ya 56 na Talisca dakika ya 90+4' ambapo kwa upande wa PSG ni Marquinhos dakika ya 43, beki Sergio Ramos dakika ya 53, Kylian Mbappe dakika ya 60 kwa penati na Ekitike dakika ya 78.

Baada ya mechi hiyo kumalizika Ronaldo amesema; "Nimefurahi kurejea tena uwanjani na kwenye orodha ya wafungaji, ni furaha kukutana na baadhi ya marafiki zangu wa zamani."

Huenda hii ikawa mechi ya mwisho inayokutanisha mshindi mara 5 wa Ballon D'or (Ronaldo) dhidi ya mshindi mara 7 wa tuzo hiyo (Messi).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live