Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uamuzi mdogo hatma uchaguzi TFF Julai 16

Mahakama Pic Data Uamuzi mdogo hatma uchaguzi TFF Julai 16

Fri, 9 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Jaji Edwin Kakolaki ametumia saa 4 kusikiliza kesi ndogo namba 305 ya kusimamisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) ambayo amesema ataitolea uamuzi Julai 16, saa 8:00 mchana.

Ally Salehe miongoni mwa wagombea urais kwenye uchaguzi huo aliyeenguliwa kwenye hatua za awali kwa kutokidhi takwa la kikanuni alifungua kesi Mahakama Kuu kupinga mchakato huo sanjari na katiba ya TFF.

Awali kesi hiyo ilisikilizwa kwa mara ya kwanza Julai 3 na leo imesikilizwa kwa mara ya pili kuanzia saa 3:18 asubuhi hadi saa 7:00 mchana alipoeleza kuitolea uamuzi Julai 16.

Nje ya Mahakama, Wakili Frank Chacha anayemtetea Ally Salehe amesema kila upande umepeleka hoja zao na wanachosubiri ni uamuzi wa Mahakama katika kesi ndogo namba 305 kama mchakato wa uchaguzi huo uendelee au usitishwe.

S.Uchaguzi mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 7 mjini Tanga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz