Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UVUMI: Taarifa zasambaa kifo cha Mino Raiola

Mino Raiola Mino Raiola

Thu, 28 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kumesambaa taarifa za kifo cha Wakala maarufu wa wachezaji Barani Ulaya, raia wa Italia Mino Raiola akidaiwa kuugua kwa muda mfupi.

Wakala huyo anaewasimamia wachezaji wakubwa duniani kama Erling Haaland, Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic ana umri wa miaka 54.

Taarifa za ndani zinadai kuwa Raiola alilazwa kwa mara ya kwanza jijini Milan na kufanyiwa upasuaji nyeti ambao mwisho wa siku ugonjwa uliosababisha upasuaji huo haukuwekwa wazi.

Wakala huyo maarufu alifanyiwa upasuaji mwezi Januari japokuwa haikuwekwa wazi hasa upasauaji huo ulikua kwa ugonjwa gani.

Baada ya kufanyiwa upasuaji inasemekana hali yake haikuwa mbaya kiasi kwamba alipewa muda wa mapumziko kwa ajili ya kuimarika.

Baadhi ya Wachezaji anaowasimamia ni pamoja na Matthijs de Ligt, Gianluigi Donnarumma, Marco Verrati, Henrikh Mkhitaryan.

Hata hivyo vyombo kadhaa vya habari kutoka Barani Ulaya vimekanusha taarifa hiyo vikisema yupo mahututi na hajakumbwa na mauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live