Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023 kuzinduliwa

UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023 Kuzinduliwa UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023 kuzinduliwa

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashindano ya UVCCM Dr. Samia Football Super League 2023 Wilaya ya Shinyanga Mjini yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 26, 2023 yakiongozwa na kauli mbiu "SHINYANGA BALL LIMERUDI",ambapo fomu za usajili kwa timu zitakazoshiriki zitaanza kuchukuliwa Agosti 9 2023 na kurudishwa Agosti 16 2023 na jumla ya timu zitakazoshiriki mashindano hayo ni Timu 32.

Akisoma taarifa kwa Viongozi wa Timu kwenye kikao kilichofanyika Agosti 08 2023 katika ukumbi wa CCM Wilaya Shinyanga mjini, Katibu wa Uhamasishaji UVCCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Samson Suleiman amesema siku ya kuzinduliwa mashindano hayo kutakua na zoezi la kugawa jezi kwa Timu shiriki na ratiba ya mashindano itatolewa.

Suleiman amesema kuwa mashindano yatakuwa ya mtoano (Knock out) huku timu zitakazoshiriki ni 32 na baada ya hatua ya mtoano zitatakiwa kubaki timu 16 ambazo zitagawanyishwa kwa makundi manne (4) (kila kundi litakuwa na timu (4)) ambapo kila kundi litatoa timu mbili (2) kwa ajili ya kuingia hatua ya robo fainali.

“Baada ya kuingia hatua ya robo fainali litafunguliwa dirisha dogo kw aajili ya kufanya usajili kwa timu zeye uhitaji,mashindano haya yanashirikisha makundi maalum (Boda Boda,Wafanyakazi wa Sokoni,Wanafunzi wa vyuo kama VETA,chuo cha Kolandoto,S.t Joseph,Shy com na Mwasele”,amesema Suleiman.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashindano Wilaya Shinyanga Mjini, Jackline Isaro amesema mashindano hayo ni tija na fursa kwa vijana sambamba na kusisitiza nidhamu kwenye michezo hali itakayosaidia kupata ushindi na zawadi mbali mbali kwa timu hadi kwa mchezaji mmoja mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live