Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UTABIRI: Ten Hag ndie Kocha anaefuata kutimuliwa

Ten Hag Majeruhi.png Kocha wa Man United, Erik Ten Hag

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti zinadai kocha wa Manchester United Erik Ten Hag yupo kwenye nafasi yapili katika orodha ya makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kufukuzwa kwenye EPL kwa msimu huu.

Kocha huyo raia wa Uholanzi ametumia kiasi cha Pauni 200 milioni katika dirisha lililopita la usajili lakini hadi sasa mambo yanaonekana kuwa mabaya kwa upande wake.

Hadi sasa kocha huyu amepoteza mechi nne kati ya saba za Ligi Kuu England na hivi karibuni mambo yameonekana kuwa mabaya kwao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ambako wamepoteza mechi mbili mfululizo ikiwa inaburuza mkia kwenye msimamo wa kundi A.

Ten Hag amewekwa kwenye nafasi yapili kati ya wale wanaopewa nafasi kubwa ya kufukuzwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na kampuni ya Sky Bet.

Mbali ya Ten Hag kocha anayeshika nafasi kwa mujibu wa utafiti huo ni Paul Heckingbottom wa Sheffield United ambaye timu yake ipo mkoni mwa msimamo wa ligi.

Kocha wa Everton Sean Dyche naye anashika nafasi yatatu akifuatiwa na Andoni Iraola wa Bournemouth na Gary O'Neil anayeinoa Wolves.

Kiujumla Man United imepoteza mechi sita kati 10 za michuano yote ilizocheza hadi sasa ikiwa imeshinda dhidi ya Wolves, Nottingham Forest, Burnley na Crystal Palace pekee.

Licha ya baadhi ya mashabiki kutokuwa na imani naye na kutaka afukuzwe, Ten Hag, haonekani kuwa na hofu juu ya hatma yake na kusisitiza kwamba viongozi na wafanyakazi wote kwa ujumla wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu kuhakikisha wanairudisha timu kwenye ubora wake.

"Msimu uliopita, ulikuwa mzuri kiasi, tupo kwenye kipindi cha mpito na tulifahamu kwamba tutapitia kwenye nyakati ngumu kama hizi."

Mechi ya mwisho kwa mashetani hawa wekundu kupoteza ilikuwa ni dhidi ya Galatasaray kwenye Ligi ya Mabingwa ambapo ilifungwa 3-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live