Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

USJAJILI: Wakongo Yanga gumzo jipya

Wacongo Pic Data Wachezaji Yanga

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

YANGA ijayo ndani silaha, nje silaha, kwani imeshusha majina mazito yanayojua kazi uwanjani lakini kubwa linalojadiliwa na wadau wengi ni jinsi ilivyojaza wachezaji wengi kutoka DR Congo.

Yanga hadi sasa ina mastaa watano kutoka Congo na baadhi yao wameshacheza pamoja kwenye ligi sambamba na timu ya taifa.

Straika wao kipenzi aliyerejea Jangwani, Heritier Makambo ‘Mzee wa Kuwajaza’ jana alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Yanga huku pia taarifa zikisema Fiston Mayele na Djuma Shabani, wameshasaini mikataba na wataungana na Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda ambao walikuwepo msimu uliopita.

Wachezaji hao karibu wote isipokuwa Makambo walishawahi kucheza timu moja AS Vita pamoja na timu ya Taifa ya Congo hivyo pengine haitakuwa ngumu kupata muunganiko wakishuka pamoja kikosini Yanga msimu ujao.

SIRI IKO HAPA

Kucheza kwa kiwango cha juu kwa nyota waliosajiliwa na Yanga kutokea nchi ya Congo katika siku za karibuni kumetajwa kuwa ni siri ya klabu hiyo kuvutika kuwaleta wakali zaidi kutokea nchi hiyo iliyojaa vipaji vilivyosambaa hadi katika ligi kubwa za soka za Ulaya.

Makambo aliifungia Yanga mabao 17 msimu wa 2018-19 na hata David Molinga Falcao licha ya kuonekana na mwili mkubwa alifunga mabao 15 ya michuano yote msimu wa 2019-20, huku pia Mukoko na Tuisila wakipiga shoo ya maana msimu uliopita.

Wachezaji kutoka Congo wanatajwa kuwa hawatowaangushi wanaYanga licha ya hivi karibuni mashabiki wa timu hiyo kutovutiwa na huduma ya kipa kutoka taifa hilo, Klaus Kindoki.

Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula alisema upepo sasa ni Congo baada ya Uganda na Kenya huku akiweka wazi kuwa tangu timu hiyo imeanza kusajili nyota kutoka nchi hizo hawajawahi kuwaangusha.

“Ni wachezaji wengi lakini kwa soka hakuna shida, kinachoangaliwa ni ubora kama wataweza kuibeba Yanga msimu huu baada ya kushindwa kufanya vizuri na kukosa taji ndani ya misimu minne mfululizo,” alisema.

Nyota wa zamani wa Yanga, Said Maulid ‘SMG’ alisema timu kusajili wachezaji wengi kutoka nchi moja haina shida na sio mara ya kwanza kutokea huku akiweka wazi kuwa ubora ndio silaha ya mafanikio.

“Sasa naona upepo upo Afrika sana, timu nyingi zimesajili nyota kutoka Congo, ishu ya Yanga kujaza Wacongo wengi sitaki kuizungumzia sana kwa sasa kwasababu sijawaona wote wakicheza kwenye ligi yetu, lakini waliopewa nafasi hadi sasa wamethibitisha ubora.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz