Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

US Monastir waiachia Yanga kuongoza kundi D

Monastir Dsf.jpeg US Monastirienne

Mon, 3 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji US Monastirienne wamekamilisha mechi zao za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya AS Réal Bamako ya Mali Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi mjini Radès, Tunis nchini Tunisia.

Mabao ya Monastir yamefungwa na beki Mtunisia, Saleh Harabi dakika ya 35 na mshambuliaji Mualgeria, Abdelhakim Amokrane dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Real Bamako limefungwa na kiungo wa Mali, Makan Samabaly.

Kwa matokeo hayo, AS Real Bamako inafikisha pointi 13, Sawa na Yanga ya Tanzania ilioongoza Kundi kwa wastani mzuri wa mabao.

Timu nyingine zilizoongoza nakundi mbali na Yanga ni; Marumo Gallants ya Afrika Kusini (A), ASEC Mimosas ya Ivory Coast (B) na FAR Rabat ya Morocco C.

Ziliomaliza nafasi ya pili mbali na Monastir ni USM Alger ya Algeria (A), Rivers United ya Nigeria (B) na Pyramids ya Misri (C).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live