Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UPDATES: Simba, Coastal hakuna mbabe kipindi cha kwanza

FDCsYz3WQAMEvBK (600 X 400) Simba vs Coast bado suluhu

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka Uwanja wa Benjamin Mkapa, dakika 45 za mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Coastal Union zimemalizika kwa suluhu (0-0).

Mechi ilianza kwa timu zote mbili kucheza kwa tahadhari kwa mpira wa taratibu na kushambuliana kwa kushitukiza na hadi kufika dakika ya 10 kila timu ilikuwa imefanya jaribio la kupata bao katika lango mwenzake.

Namna dakika zilivyozidi kwenda, kasi ya mchezo ilizidi kuongezeka ambapo kuanzia dakika ya 25 hadi 28 Coastal ilimiliki mpira kwenye eneo la Simba ikitafuta bao lakini mbinu zao ziliishia kwa mabeki wa Simba wakuongozwa na Henock Inonga.

Sekunde chache baadae Simba nayo ikiongozwa na Kibu Denis, Rally Bwalya na John Bocco ilifanya mashambulizi matatu mfululizo ambayo yote hayakuipa bao timu hiyo.

Baada ya Simba kuona ngome ya Coastal ipo imara na mara nyingi kujikuta wakiotea, kuna muda walibadili aina yao ya uchezaji na kuanza kupiga mashutu ya mbali ambayo nayo hayajafanikiwa kuwapa bao.

Dakika ya 31, mashabiki wa Simba waliopo uwanjani hapo walishangilia na kupiga makofi kwa wingi pale kiungo wao wa muda mrefu Jonas Mkude alipoinuliwa kwenye kiti na kwenda kupasha misuli joto na dakika ya 44 aliingia kuchukua nafasi ya Muzamiru Yassin aliyeumia.

Muda huo huo, Simba ilifanya mabadiliko mengine ya lazima kwa kumuingiza Benard Morrison kuchukua namba ya Sadio Kanoute aliyeumia wakati sawa na Muzamiru baada ya kugongana na wachezaji wawili wa Coastal katikati ya Uwanja.

Jacob Benedicto wa Coastal Union ndiye mchezaji pekee aliyeoneshwa kadi ya njano katika dakika 45 za kipindi cha kwanza ambazo zimemalizika kwa suluhu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live