Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UMISETA ni balaa huko Tabora

Umisetaaa Es (4).jpeg Umiseta

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa jana Mashindano ya 28 ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISETA) yakifunguliwa, tayari mikoa kadhaa imeanza vizuri safari ya kuwania ubingwa wa michezo hiyo inayofanyika mkoani Tabora. Michezo ya UMISETA imeta

Katika michezo ya awali hatua ya makundi kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana, wenyeji Tabora wameaachapa Kigoma pointi 48-24, Dodoma ikilala kwa Mbeya kwa pointi 51-29.

Kwenye mchezo wa mpira wa wavu wasichana Katavi imefungwa na majirani zao Rukwa kwa seti 0-3, Manyara imeichapa Dodoma kwa seti 3-0 wakati kwa upande wa wavulana Dar es Salaam wameichapa Arusha kwa seti 3-0 huku Mara ikiishia Mtwara kwa seti 2-1.

Katika mchezo wa mpira wa mikono wasichana, Manyara imeishinda Njombe mabao 11-10, Pwani ikilala dhidi ya Kagerea kwa mabao 24-12 na Tabora ikiwafunga Kilimanjaro kwa mabao 32-18.

Kundi B Shinyanga ilikuwa hoi kwa Mbeya kwa mabao 23-11 na Dar es Salaam ikiishinda Katavi mabao 18-12 huku kwa kindi V Tanga ikiichapa Mwanza kwa mabao 23-12 na Singida ikiishinda Rukwa mabao 13-12 wakat kundi D Mara ikiishinda Kigoma mabao 22-16 na Iringa ikiishinds Lindi kws mabao 12-8.

Katika mchezo wa soka wavulana, Uguja imetoka suluu na Kilimanjaro na Morogoro ikiibuka kidedea kwa mabao 3-1dhidi ya Iringa.

Pia Singida imeichapa Arusha kwa mabao 2-1, Dodoma ikichoshana nguvu na Mwanza baada ya kutoka suluu na Geita ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi Mara na Mtwara ikiwachapa kwa bao 2-0.

Una maoni, tuandikie.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live