Hakika, sheria hufuata mkondo wake. UEFA imetembeza rungu la adhabu kwa baadhi ya vilabu vinavyoshiriki mashindano yake.
Mchezo wa pili kati ya Manchester United na Atletico Madrid, uligubikwa na vitendo visivyo vya kiuungwana dhidi ya kocha wa Atletico, Diego Simeone. Baadhi ya mashabiki wa United walimrushia makopo kocha huyo wakati anatoka uwanjani. United wameadhibiwa kulipa faini ya £8,420 kwa tukio hilo.
Liverpool wameambulia adhabu ya kulipa faini ya £8,420 kutokana na vitendo vilivyohusishwa na kuchelewesha kuanza kwa mchezo wa UEFA dhidi ya Benfica. Rangers pia wameadhibiwa kulipa faini ya kiasi cha £38,900 kutokana na mashabiki wa timu kuwasha moto na kuchelewesha mchezo dhidi ya Braga.
Pamoja na adhabu hizi, kocha wa Liverpool – Jurgen Klopp amepewa onyo na shirikisho hilo hasa katika maandalizi ya timu yake ambapo alihusika katika kuchelewesha muda wa mchezo kuanza.