Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UEFA ni Waingereza, Wahispania nusu fainali

Pep Pic Data UEFA ni Waingereza, Wahispania nusu fainali

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu nne za Hispania na England zitakutana katika mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa soka barani Ulaya baada ya Manchester City na Liverpool kulazimisha sare dhidi ya Atletico Madrid na Benfica katika mechi za nusu fainali jana (Jumatano).

Manchester City itakutana na Real Madrid katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa soka barani Ulaya baada ya kuiondoa Atletico Madrid jana kwa jumla ya bao 1-0, wakati vigogo wengine wa England, Liverpool watakutana na Villareal.

Bao la Kevin De Bruyne alilofunga wiki iliyopita katika mechi ya kwanza ya robo fainali kwenye uwanja wa Etihad lilitosha kuivusha timu ya Pep Guardiola baada ya mechi ya marudiano iliyofanyika jana nchini Hispania kushindwa kuzalisha goli lolote.

Manchester City imefika nusu fainali kwa mwaka wa pili mfululizo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz