Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UEFA kumzuia Mbappe kuvaa Mask yenye bendera ya Ufaransa

Mbappe France Mask Kylian Mbappe

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada kuvunjika pua kwenye mchezo wa kwanza wa makundi wa EURO 2024, nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappé amerejea kikosini na inaelezwa kuwa atacheza leo dhidi ya Uholanzi huku akiwa amevalia kifuniko kigumu cha uso cha kumlinda (barakoa).

Mbappé alionekana akiwa amevalia barakoa yenye rangi nyeupe, nyekundu, na bluu za berndera ya taifa ya Ufaransa wakati wa mazoezi mepesi na wachezaji wenzake siku ya Alhamisi lakini hataruhusiwa kuvaa barakoa hiyo kwenye mechi za EURO kwa kuwa inakiuka kanuni za UEFA

Kwa mujibu wa kanuni za UEFA, mchezaji ataruhusiwa kuvaa barakoa ya rangi moja pekee wakati wa mechi, isipokuwa kama kuna msamaha maalum.

“Vifaa vya matibabu vinavyovaliwa kwenye uwanja wa mchezo lazima viwe na rangi moja na visiwe na alama za timu au mtengenezaji,” inasomeka sehemu ya kanuni za UEFA.

Mbappé alipata jeraha hilo baada ya kugongana na beki wa Austria, Kevin Danso siku ya Jumatatu na kulazimika kutoka nje ya uwanja huku kukiwa na wasiwasi ikiwa ataweza kumaliza mechi zilizobaki za hatua ya makundi.

Ufaransa itachuana na Uholanzi leo, Juni 21 2024 kwenye mchezo wa raundi ya pili wa Kundi F utakaopigwa katika dimba la Red Bull Arena (Leipzig) majira ya saa 4:00 usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live