Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UEFA : Timu za CONMEBOL Kucheza UEFA Nation League

Uefa President Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Raisi wa UEFA, Zbigniew Boniek amethibitisha UEFA na Bodi ya Amerika Kusini CONMEBOL wamefikia makubaliano kwaajili ya Timu za America Kusini kushiriki katika mashindano ya UEFA Nations League.

Raisi huyo amesema Timu hizo za taifa kanda ya CONMEBOL zitajumuika pamoja na timu za Ulaya katika mashindano ya Nations League ya mwaka 2024.

Mashindano ya Nations League yalianza mwaka 2018 yakishirikisha mataifa 55 na sasa jumla ya mataifa 10 kutoka CONMEBOL yanatarajiwa kuongezeka katika upanuzi wa mashindano hayo mwaka 2024.

“Kuanzia mwaka 2024 CONMEBOL watajiunga Nations League” alisema Boniek.

“Hatujajua bado kwa kutumia kanuni gani, kwa fomu ipi. Tumesaini makubaliano kati ya CONMEBOL na UEFA na kuanzia mwaka 2024 timu hizi zitashiriki mashindano ya Nations League.” aliongeza.

Boniek aliongeza kwamba timu sita za amerika kusini zitajiunga na Kundi A la Nations League wakati nyingine nne zitajiunga Kundi B. mashindano yanatarajiwa kuchezeka Ulaya ili kupunguza gharama za usafiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live