Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UEFA Nations League kuziba pengo la World Cup

Uefa Nation Ligi TROPHY Kombe la Ligi ya Mataifa ya Ulaya, chini ya shirikisho la soka Ulaya

Tue, 31 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Michuano ya UEFA Nations League ya 2022-23 inarajia kuanza Jumatano hii June 01, na mataifa yote ya Ulaya yatakua yameshacheza katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Mashindano hayo yanaziba pengo lililoachwa na michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuhamia mwezi Novemba mwaka huu tofauti inavyokuaga miaka mingine ambapo hua inafanyika mwezi June hadi Julai. Nchi za England na Ireland ya Kaskazini watacheza michezo minne ya makundi, huku Wales wakiwa na michezo minne ya makundi pamoja na fainali ya mtoano wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

(Makundi ya UEFA Nations League)

Scotland, ambao wanakutana na Ukraine katika mchezo wa nusu-fainali ya mtoano wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia Jumatano, wanakabiliwa na mechi tatu za Ligi hiyo ya Mataifa ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na dhidi ya Jamhuri ya Ireland mchezo utakaopigwa huko Dublin.

Ligi ya Mataifa ya Ulaya ni michuano inayofanyika kila baada ya miaka miwili ambapo sasa inakwenda katika msimu wake wa tatu tangu kuanzishwa kwake.Ureno ndio ilikua timu ya kwanza kutwaa taji hili katika msimu wake wa kwanza mnamo mwaka 2019 na Ufaransa ndio mabingwa watetezi msimu huu baada ya kuifunga Uhispania kwenye mchezo wa fainali ya mwaka 2021.

Chanzo: eatv.tv