Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake "Twiga Stars" kimewasili nchini kikitokea Afrika ya Kusini ilipokwenda kushiriki Mashindano ya COSAFA WOMEN 2021 CHAMPIONSHIP.
Kikosi cha Twiga Stars kiliibuka bingwa baada ya kuichapa Timu ya Malawi katika mchezo wa fainali.
Katika michuano hiyo, nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” Amina Bilali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” Bakari Shime akizungumza baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julus Nerere (JNIA) wakitokea Afrika Kusini walikotwaa ubingwa wa COSAFA Wanawake 2021 pic.twitter.com/5CY7qhjOE9
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) October 12, 2021