Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars yasonga mbele kufuzu Olimpiki Paris 2024

Twiga Stars Kikosi Vs Botswana Twiga Stars yasonga mbele kufuzu Olimpiki Paris 2024

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya wanawake’Twiga Starst’ imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Michezo ya Olimpiki mwakani Paris baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Botswana Uwanja wa Taifa Jijini Gaborone nchini humo.

Bao pekee la Twiga Stars limefungwa na mshambuliaji wa BK Häcken ya Sweden, Aisha Masaka na kwa matokeo hayo mabinti wa Tanzania wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kuilaza Botswana 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.

Sasa Twiga Stars itamenyana na Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu, ambayo imeitoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kuna jumla raundi ya Nne za mchujo na mwishowe timu mbili za Afrika zitaiwakilisha Afrika huko Paris.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live