Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars, yaifuata Namibia kulipa kisasi

Pjimage (48) Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeondoka Dar es Salaam Jumatano usiku kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Namibia Jumamosi Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg Raundi ya Kwanza kufuzu AFCON ya mwakani Morocco.

Twiga Stars imeondoka mara tu baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Namibia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam jioni ya Jumatano.

Mchezo wa marudiano kufuzu AFCON dhidi ya Namibia utakaochezwa Oktoba 23, 2021 uwanja wa Dobsonville, Soweto, Afrika ya Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live