Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars yachapwa 2-1 nyumbani

Twiga Stars Kichapo Mchezo kati ya Twiga Stars dhidi ya Namibia

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, "Twiga Stars" imechapwa mabao 2-1 na Namibia nyumbani, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, katika mchezo wa kwanza wa kufuzu AFCON ya mwakani itakayofanyika nchini Morocco.

Mabao ya Namibia yote yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Zenatha Goeieman Coleman dakika ya 22 na 61, wakati bao pekee la Twiga Stars limefungwa na kiungo wa JKT Queens, Stumai Abdallah Athumani dakika ya 41.

Timu hizo zitarudiana Oktoba 23 Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg, Afrika Kusini na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Malawi na Zambia na atakayeshinda hapo amekata tiketi ya Morocco mwakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live