Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars wakabidhiwa Mil. 10 za 'goli la Mama'

Twiga Stars Wakabidhiwa Mil. 10 Za 'goli La Mama'.jpeg Twiga Stars wakabidhiwa Mil. 10 za 'goli la Mama'

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ameikabidhi timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kiasi cha Tsh. Milioni 10 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia ushindi waliopata dhidi ya timu ya Ivory Coast.

Wakati akikabidhi fedha hizo Msigwa amesema wachezaji hao wanafanya kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi kimataifa na Serikali ipo pamoja nao kwa kuwa wanaitangaza na kuipigania nchi yao.

"Mnapokuwa uwanjani katika mechi za kimataifa mnakuwa mmebeba matumaini ya watanzania, katika mechi zote mlizocheza tumeona dhamira mliyonayo kwa nchi yenu, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapongeza sana, anafurahi sana anapowaona mnacheza uwanjani, anafurahi sana mnapopata matokeo mazuri katika mechi zetu,” amesema Msigwa.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime amesema amefurahi kupokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Rais Samia ambazo ni Hamasa kwa vijana hao kujituma zaidi kupambania nchi yao lakini kubwa kwa vijana hao ni pale kuona Rais anatambua mchango wao.

"Fedha ni sehemu kubwa ya hamasa, kitendo cha Rais Samia kuwafuatilia vijana wetu na kutambua timu hiyo inacheza ni faraja kubwa l na imekuwa chachu ya kujituma wakiamini kuwa Mama yupo pamoja nao," amesema Shime.

Aidha nahodha wa Twiga Stars, Joyce Lema amesema wanamshukuru Rais Samia kwa kuzidi kuwapa hamasa na kumuahidi kutomuangusha katika mashindano yote yaliyopo mbele yao.

"Kwa hamasa hii inaonyesha kuwa kuna kitu kimeongeza katika soka la wanawake, tunatamani siku moja viongozi kuendelea kujitokeza kwa wingi kusapoti soka la wanawake kama ilivyo kwa wanaume,” amesema Joyce.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live